Mtahiniwa anatakiwa kuomba uthibitisho wa matokeo ambao utapelekwa kwa
mwajiri au katika taasisi anayotaka kwenda kusoma. Lakini pia mtahiniwa
anaweza kuomba nakala ya matokeo (Result Slip) yenye uthibitisho. Hii ni
nyaraka ya kiofisi inayotolewa NECTA ambayo huonesha daraja alilopata
mtahiniwa katika mtihani husika. Uthibitisho wa nakala ya matokeo
utakubaliwa na taasisi za elimu na hata sehemu mbalimbali za ajira kama
kumbumbukumbu halali ya matokeo ya mtihani.

Comments
Post a Comment