Skip to main content

Sababu gani zinafanya matokeo ya watahiniwa kuzuiwa na misimbo gani inatumika?

* S: Matokeo yamesitishwa hadi uthibitisho wa kasoro zilizoonekana ama katika kuingiza taarifa, kushiriki katika masuala ya uvunjaji wa kanuni au ukiukaji wa maadili katika mitihani. Matokeo yaliyositishwa kutokana na vituo au shule kushindwa kukidhi masharti ya usajili (yaani vituo vyenye watahiniwa chini ya 35)..
* E: Matokeo yamezuiwa, mpaka upatikane uthibitisho wa mtahiniwa kulipa ada ya Mitihani.
* I: Matokeo HAYAJAKAMILIKA kutokana na mtahiniwa kukosa alama za Upimaji Endelevu (CA) katika masomo yote aliyofanyia mtihani.
I: Matokeo hayajakamilika kutokana na kukosekana kwa alama za Upimaji Endelevu (CA) wa mtahiniwa katika somo moja au zaidi alilofanyia mtihani lakini si yote.
* W: Matokeo yamezuiwa/yamefutwa au kubatilishwa kutokana na ushahidi wa mtahiniwa kushiriki katika mambo ya kukosa uaminifu au ukiukaji wa taratibu kabla, wakati au baada ya mitihani..
* T: Matokeo yamesitishwa kutokana na mtahiniwa kujibu mtihani wa somo moja au zaidi ambalo hakusajiliwa (mtahiniwa mwizi).
ABS: Watahiniwa wanaoshindwa kufanya mitihani.
FLD: Mtahiniwa ameshindwa Mtihani.
X: Mtahiniwa hakutokea kufanya mtihani kwa somo alilosajiliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Nini cha kufanya iwapo nitakuwa nimepoteza cheti changu cha kidato cha nne?

Mtahiniwa anatakiwa kuomba uthibitisho wa matokeo ambao utapelekwa kwa mwajiri au katika taasisi anayotaka kwenda kusoma. Lakini pia mtahiniwa anaweza kuomba nakala ya matokeo (Result Slip) yenye uthibitisho. Hii ni nyaraka ya kiofisi inayotolewa NECTA ambayo huonesha daraja alilopata mtahiniwa katika mtihani husika. Uthibitisho wa nakala ya matokeo utakubaliwa na taasisi za elimu na hata sehemu mbalimbali za ajira kama kumbumbukumbu halali ya matokeo ya mtihani.

CHECK NECTA PSLE 2019 RESULTS HERE

Check All Necta Results Below 2019 PSLE /Standard Seven RESULTS

Habari - News

CLICK HERE FOR Habari - News